• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNPD yasema serikali ya Uganda inafaa kulenga watalii 10m kufikia ukuaji

    (GMT+08:00) 2018-11-14 18:44:24
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) limeitaka serikali ya Uganda kuongeza malengo yake ya utalii ili kupata fedha za kigeni kwa ajili ya maendeleo.

    Akizungumza wakati wa mapitio ya tisa ya sekta ya utalii,Muwakilishi wa UNDP nchini Uganda Bi Rose Malango, alisema uwekezaji zaidi unatakikana katika sekta ya utalii iwapo nchi hiyo inataka kufikia malengo ya kitaifa ya maendeleo.

    Kulingana na takwimu za mwaka 2017 kutoka Wizara ya Utalii,utalii ni chanzo kikuu cha fedha za kigeni nchini humo,ukiingiza $1.453b.Sekta hiyo inachangia takriban asilimia 7.3 kila mwak katika pato la taifa.

    Kwa mujibu wa Waziri wa Utalii Prof Ephraim Kamuntu,idadi ya watalii iliongezeka kutoka 1.4 milioni hadi 1.62 milioni mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako