• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Waziri mpya Japhet Hasunga asimamia shughuli ya ununuzi wa korosho Mtwara

    (GMT+08:00) 2018-11-14 18:44:40
    Waziri mpya wa Kilimo nchini Tanzania Japhet Hasunga na Naibu Wake Innocent Bashungwa wamekita hema Mtwara kusimamia uhakikiso wa data na malipo kwa wakulima wa korosho,shughuli ambayo imeanza leo kufuatia uamuzi wa serikali wa kununua zao la korosho kwa Sh3,300 kwa kilo.

    Hasunga alisema malipo ya korosho yataanza kuonekana katika akaunti za benki za wakulima leo baada ya shughuli ya uthibitishaji.

    Aidha alisema kuwa hataondoka Mtwara hadi ahakikishe kuwa amevikabidhi vyama vya ushirika hundi na kwamba pesa zinawekwa kwenye akaunti za benki za wakulima.

    Pia aliwaomba wakulima kuwa na subra kwani sio wote watakaolipwa leo,lakini alitoa hakikisho kwamba kila mmoja atalipwa baada ya shughuli ya uthibitishaji.

    Siku ya jumatatu Rais Magufuli alikikabidhi kiwanda kikuu cha uchakataji korosho cha Lindi cha Bucco Investment Holdings Factory kwa jeshi kutoka kwa wawekezaji binafsi.Alilipatia jeshi jukumu la kusimamia uchakataji na usafirishaji wa korosho.

    Pia alitoa agizo la minada yote ya korosho kufungwa ,akisema kuwa serikali yake itanunua tani 90,000 za korosho ambazo zimesalia kwa wakulima kwa muda sasa kutokana na mgogoro wa bei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako