• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yaya Toure arudi Olympiakos, atambulishwa kwa mashabiki

    (GMT+08:00) 2018-11-15 08:36:34
    Kiungo nyota wa zamani wa Ivory Coast, Yaya Toure amerejea kwenye klabu yake ya kwanza ya Olympiakos ya Ugiriki.

    Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Manchester City amesema amepokea ofa kutoka klabu mbalimbali za Ulaya, Asia na Marekani na kuzitolea nje akiamua kurejea kwenye klabu hiyo iliyomuibua katika msimu wa mwaka 2005/2006.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amesema ametimiza ahadi aliyoiweka mwaka 2006 wakati anaodnoka katika klabu hiyo, na kuwa anaifahamu vizuri ligi ya Ugiriki na namna ushindani ulivyo hivyo hahitaji kutoa ahadi nyingi za maneno bali anaiachia miguu yake kueleza amerudi na nini. timu hiyo imeuzu michuano ya ligi ya Ulaya baada ya kuicabanga Burnley ya Uingereza kwa jumla ya goli 4-2 katika mchezo wa mtoano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako