• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Maonyesho ya kibiashara kati ya Kenya na China yaingia siku ya pili

    (GMT+08:00) 2018-11-15 16:55:29

    Hii leo ni siku ya pili tangu kufunguliwa rasmi kwa maonyesho ya kibiashara kati ya China na Kenya. Maonyesho haya ambayo yanafanyika katika ukumbi wa jumba la mikutano ya kimataifa, KICC yameleta pamoja mamia ya kampuni za Kichina na ambazo zina matawi yake nchini Kenya. Kupitia warsha hiiya siku nne, wakenya na wageni kutoka mataifa mengine watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali kando na kujifunza mengi kuhusiana na bidhaa za teknolojia ya hali ya juu. Waziri wa biashara wa Kenya Bwana Peter Munya alisisitiza umuhimu wa ushirikianao wa kibiashara uliopo kati ya Kenya na China, na kusisitiza kuwa Kenya itazidi kuboresha mazingira ya kibiashara kwa wawekezaji zaidi wa kigeni. Vile vile, alidokeza kuwa kampuni za China zimejihusisha pakubwa na ujenzi wa miradi mikubwa iliyopo Kenya. Akitoa mfano wa Reli mpya ya kisasa ya SGR, waziri Munya alisema kuwa Kenya inajivunia sana kuwa kwenye uhusiano wa karibu na taifa la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako