• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuunga mkono viwanda binafsi yenye sifa bora kuvuta mitaji kwa kuuza hisa

    (GMT+08:00) 2018-11-15 17:29:40

    Ili kutatua masuala ya kuvutia mitaji yaliyovikumbwa na viwanda binafsi, msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bibi Meng Wei, amesema China itachunguza na kutoa sera na hatua za kuvisaidia viwanda binafsi kuvuta mitaji kwa kuuza hisa. Fadhili Mpunji ana zaidi.

    Msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bibi Meng Wei, amesema China itaunga mkono viwanda binafsi vyenye sifa bora ambavyo vinajiendeleza vizuri, na kuongoza kuinua miundo ya viwanda na uchumi wa kikanda, na kuvisaidia kutoa ombi la kuuza hisa kwa mujibu wa sera husika za kuvuta mitaji moja kwa moja.

    "kwa viwanda binafsi vyenye sifa bora, tunasimamia matumizi ya fedha za hisa kwa orodha hasi, kuhimiza kutumia fedha za hisa katika mkakati mkubwa wa taifa, sekta muhimu na miradi mikubwa. Hivi karibuni kamati yetu imeidhinisha kampuni ya BYD kuuza hisa zake zenye thamani ya yuan bilioni 6, fedha hizo zitatumika katika miradi isiyochafua mazingira kama vile magari ya nishati mpya, betri na vifaa vya kutengenezea betri, na treni inayotumia njia moja."

    Aidha, kamati ya maendeleo na mageuzi ya China pia itaongeza uungaji mkono kuuza hisa za viwanda vipya, kuratibu shughuli za viwanda binafsi kushindwa kulipa hisa kwa wakati, ili kuvisaidia viwanda hizo kukabiliana na taabu.

    "Kamati yetu inatoa msaada wa kifedha kwa viwanda binafsi vinavyoshindwa kulipa hisa kwa wakati kutokana na upungufu wa fedha, lakini zinaendana na mwelekeo wa kuboresha miundo ya uchumi na vyenye mustakabali mzuri. Kuondoa hatari inayotokana na kushindwa kulipa hisa, kuvisaidia viwanda binafsi muhimu katika sekta fulani, vinazotoa nafasi nyingi za ajira na za sekta mpya kwa njia ya soko na kisheria. "

    Bibi Meng pia amesema, kamati hiyo pia itashirikiana na idara za usimamizi wa mambo ya fedha, kutekeleza mpango wa kuvutia mitaji kwa njia ya uuzaji wa hisa, kuunga mkono viwanda binafsi vinazovyoendeshwa vizuri, lakini vina matatizo ya mzunguko wa fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako