• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uungaji mkono wa Baraza la mawaziri la Uingereza kuhusu Brexit waonyesha maendeleo muhimu ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-11-15 18:23:36

    Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mazungumzo ya Brexit Bw. Michel Barnier amesema makubaliano ya Brexit kuungwa mkono na baraza la mawaziri la Uingereza kunaonyesha mazungumzo ya Brexit yamepata maendeleo makubwa.

    Akizungumza mjini Brussels hapo jana, Bw. Barnier amesema hatua hiyo inamaanisha kuwa mazungumzo ya Brexit yamepata maendeleo makubwa, na amependekeza nchi wanachama wa Umoja huo kufanya mkutano maalumu kuhusu suala hilo mwishoni mwa mwezi huu.

    Bw. Barnier amesema, ingawa mchakato wa Brexit unakabiliana na uwezekano wa mabadiliko, lakini baada ya kufanya mzungumzo ya miezi 17, pande hizo mbili zilifikia makubaliano yenye mambo sahihi na halisi, ambayo yatatoa uhakika wa kisheria kwa kila mtu na kukabiliana na matokeo yanayosababishwa na Brexit katika pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako