• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Syria azikaribisha kampuni za China kushiriki katika ukarabati wa kiuchumi wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2018-11-15 19:33:14

    Rais Bashar al-Assad wa Syria amezikaribisha kampuni za China kuwekeza nchini humo na kushiriki kwenye ukarabati wa kiuchumi wa nchi hiyo.

    Rais al-Assad amesema hayo hivi karibuni wakati akipokea hati ya utambulisho wa balozi mpya wa China nchini Syria Bw. Feng Biao. Amesema tangu Syria na China zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 62 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa kwa utulivu, na ameishukuru China kwa kushika msimamo wa haki katika suala la Syria.

    Bw. Feng amesema, tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kibalozi, ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili katika sekta mbalimbali umeendelezwa kwa madhubuti. China inaunga mkono juhudi inayofanywa na serikali ya Syria katika kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi, huku ikiendelea kutoa mchango katika utatuzi wa kisiasa wa suala la Syria. Pia ametaka ushirikiano na mawasiliano ya kirafiki kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya na makubwa zaidi chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako