• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kuchukua hatua ya kujibu kama Marekani ikiongeza ushuru dhidi ya magari kutoka Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-11-15 19:18:49

    Mjumbe wa biashara ya Umoja wa Ulaya Bibi Cecilia Malmstrom huko Washington amesema, kama Marekani itaongeza ushuru dhidi ya magari kutoka nchi za Umoja wa Ulaya, Umoja huo utachukua hatua ya kulipiza kisasi, na sasa unafanya maandalizi kwa ajili ya hatua hizo.

    Bi Malmstrom amesema hayo baada ya mkutano na mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer. Pia amesema, Umoja huo unaandaa orodha ya bidhaa zitakazochukuliwa hatua ya kulipiza kisasi.

    Bi Malmstrom ameongeza kuwa, kutokana na ofisi ya mjumbe wa biashara wa Marekani inatakiwa kumaliza mchakato wa kufanya mazungumzo na bunge la nchi hiyo, na Umoja wa Ulaya unahitaji idhini ya mazungumzo inayotolewa na nchi wanachama, hivyo mambo halisi ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili utathibitishwa mwanzoni mwa mwaka ujao. .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako