• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kuhimiza mazungumzo ya RCRP

    (GMT+08:00) 2018-11-15 19:19:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying hapa Beijing amesema, China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kuendelea kuhimiza mazungumzo ya "Mkataba wa Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Pande Zote wa Kikanda" (RCEP) kwa kufuata kanuni za kuheshimiana na kuelewana, ili kuwanufaisha watu wa kanda hiyo mapema iwezekanavyo.

    Mkutano wa pili wa viongozi wa RCEP umefanyika jana huko Singapore na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri mkuu wa China, Li Keqiang. Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema, mazungumzo ya RCEP yamepata maendeleo halisi na pande mbalimbali zimeonesha nia ya kufikia makubaliano mwakani.

    Bi Hua amesema, mazungumzo ya RCEP ni mazungumzo makubwa na muhimu zaidi katika sehemu ya Asia na Pasifiki. Kama makubaliano hayo yakifikiwa, yatafunika nusu ya watu na theluthi moja ya biashara duniani. Wakati huohuo, sehemu hiyo itakuwa eneo la biashara huria lenye watu wengi zaidi, nchi wanachama wengi zaidi na uhai mkubwa zaidi wa kimaendeleo duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako