• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakopaji mikopo ya nyumba wapungua

    (GMT+08:00) 2018-11-15 20:41:00

    Licha ya uhitaji wa nyumba 200,000 kila mwaka ili kuondoa upungufu wa nyumba milioni tatu nchini, idadi ya watu wanaojitokeza kuchukua mikopo ya viwanja imezidi kupungua kila mwaka. Hayo yalisemwa jana na mkuu wa idara ya biashara na masoko wa Benki ya Amana, Munir Rajab katika maadhimisho ya miaka mitatu ya utoaji mikopo ya viwanja unaofanywa na benki hiyo wakishirikiana na kampuni ya Property International Ltd (PIL). Rajab alisema licha ya kuwekeza zaidi ya Sh9 bilioni katika utoaji viwanja hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu, mwamko mkubwa ulikuwa katika mwaka wa kwanza na ulizidi kushuka kadri siku zilivyosogea.

    Pia, wametoa punguzo la Sh1,000 kwa kila mita ya mraba watakaonunua wakati wa msimu wa wiki ya huduma kwa wateja unaotarajiwa kuanza Novemba 19 hadi 24. Naye ofisa mkuu wa uendeshaji wa PIL, George Obado alisema katika miaka mitatu zaidi ya wateja 1,000 wamepata mikopo ya viwanja jijini Dar es Salam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako