• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza aahidi kuendelea na mpango wake wa Brexit

    (GMT+08:00) 2018-11-16 09:12:20

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May ameahidi kuendelea kutekeleza mpango wake wa Brexit kwenye msingi wa rasimu ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, na kusema kuwa "mwelekeo anaoongoza ni sahihi".

    Akiongea na wanahabari ofisini kwake mjini London, Bibi May amesema ataendelea na mpango wake wa Brexit unaotoa kipaumbele kwa maslahi ya watu, licha ya upinzani mkubwa kutoka ndani ya chama chake na bunge.

    Rasimu hiyo ya makubaliano iliyotolewa Jumanne na Umoja wa Ulaya mjini Brussels, ni maendeleo ya kiufundi yaliyopatikana baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa miezi kadhaa kati ya pande hizo mbili kuhusu jinsi Uingereza itakavyojitoa Umoja wa Ulaya Machi 28 mwakani.

    Makubaliano hayo bado yanahitaji kupitishwa na Bunge la Uingereza na kuidhinishwa na nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako