• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa wito wa kudumisha amani na ustawi wa Asia Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-11-16 09:30:24

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang jana alihudhuria mkutano wa kilele wa 13 wa nchi za Asia Mashariki nchini Singapore akitoa wito kwa nchi zote za kanda hiyo kuimarisha mazungumzo ya usawa na kufunguliana milango, ili kudumisha amani na ustawi katika Asia Mashariki.

    Bw. Li amesema mkutano huo wa kilele ulioanzishwa miaka 13 iliyopita umekuwa jukwaa muhimu kwa mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi za Asia Mashariki.

    Wakati huo huo, Bw Li Keqiang jana alikutana na rais Vladimir Putin wa Russia kando ya mikutano ya ushirikiano ya viongozi wa Asia Mashariki, na kusema matokeo mapya yamepatikana katika ushirikiano kati ya China na Russia kwenye sekta mbalimbali, lakini bado kuna nafasi kubwa ya ushirikiano wa kiutendaji kati ya nchi hizo mbili.

    Mkutano wa kilele wa Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki na mikutano ya ushirikiano ya viongozi wa Asia Mashariki ulifungwa jana nchini Singapore, na kuhimza ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako