• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jimbo la Idlib, Syria lakabiliwa na hatari kubwa la kutokea mapambano makali

    (GMT+08:00) 2018-11-16 09:45:25

    Mshauri mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya Syria Jan Egeland amesema, ingawa hali ya jimbo la Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria imetulia kwa miezi miwili, dalili zinaonesha mapambano ya kumwaga damu yanaweza kutokea, kama mafanikio hayatapatikana katika mazungumzo kati ya makundi mbalimbali.

    Bw. Egeland pia amesema Russia na Uturuki zote zimeahidi kutochukua hatua za kijeshi kama kambi zao za kijeshi hazitashambuliwa ili kuepuka hali ya mvutano kuendelea kuwa mbaya.

    Habari zinasema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bibi Maria Zakharova, amesema jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani limefanya mashambulizi mengi katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi ukingo wa mashariki wa mto Euphrates, Syria, lakini mashambulizi hayo yaliyotumia mabomu ya phosphorus ni holela, na yamesababisha vifo na majeruhi kwa raia zaidi ya 60 katika kijiji cha al-Shafa, mashariki mwa jimbo la Deir ez-Zor.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako