• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lalaani mauaji ya walinzi amani wa Umoja wa Mataifa na askari wa jeshi la taifa nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-11-16 10:09:49

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya wanajeshi zaidi ya 20 kwenye operesheni dhidi ya waasi katika mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Kwenye taarifa iliyotolewa kwa wanahabari, wajumbe wa Baraza la Usalama wametoa salamu za pole kwa familia za waliouawa wakiwemo walinzi amani saba kutoka Malawi na mmoja kutoka Tanzania, na wengine zaidi ya 12 ambao ni wanajeshi wa DRC, na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

    Wanajeshi hao waliuawa Jumatano kwenye operesheni ya pamoja za Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kama MONUSCO, na vikosi vya majeshi vya DRC dhidi ya kundi la waasi la ADF lililopo nchini DRC na Uganda katika eneo la Beni, Kivu Kaskazini.

    Eneo la mashariki mwa DRC linasumbuliwa na uasi uliodumu kwa miaka 20, na mwaka jana wimbi kubwa la mashambulizi liliikumba Kivu Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako