Rais wa China ahudhuria uzinduzi wa shule ya Butuka nchini Papua New Guinea iliyojengwa kwa msaada wa China
(GMT+08:00) 2018-11-16 16:13:12
Rais Xi Jinping wa China na waziri wa Papua New Guinea Bw. Peter Oneil leo wamehudhuria hafla ya uzinduzi wa shule ya Butuka iliyoko kwenye bandari ya Moresby iliyojengwa kwa msaada wa China.
Rais Xi amesema katika miaka ya karibuni, mawasiliano kati ya China na Papua New Guinea katika mawasiliano kati ya watu na watu na sekta ya elimu yameimarishwa siku hadi siku, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeendelea vizuri. Amesema China inapenda kuzidisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili na kuweka msingi thabiti kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo.
Rais Xi Jinping pia amekutana na gavana mkuu wa Papua New Guinea Bw. Bob Dadae, ambaye amesema nchi hiyo inataka kufanya juhudi pamoja na China kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili.