• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Papua New Guinea zakubaliana kujenga uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote

    (GMT+08:00) 2018-11-16 17:14:26

    Rais Xi Jinping wa China leo amefanya ziara huko Port Moresby, mji mkuu wa Papua New Guinea, ambapo amekutana na gavana mkuu wa nchi hiyo Bob Dadae, waziri mkuu Peter O'Neill. Viongozi hao wamekubaliana kujenga uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbilikwa kuheshimiana na kujiendeleza kwa pamoja.

    Rais Xi Jinping alipokutana na gavana mkuu wa Papua New Guinea amesisitiza kuwa, China inafuatilia kwa ukaribu uhusiano kati yake na Papua New Guinea, anatumai ziara yake hiyo kusaidia kuinua zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kuhimiza ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili kupata matokeo makubwa. Amesema China inashikilia kuimarisha ushirikiano na mshikamano kati yake na nchi za visiwa vya Pasifiki. Gavana mkuu Bob Dadae ameishukuru China kutoa msaada kwa Papua New Guinea katika ujenzi wa miundo mbinu, elimu na sekta nyingine za maendeleo ya taifa na maisha ya raia, na kuunga mkono nchi hiyo kuendesha mkutano usio rasmi wa viongozi wa APEC. Rais Xi Jinping pia amekutana na waziri mkuu Peter O'Neill. Amesisitiza kuwa, Papua New Guinea ni nchi ya kwanza ya visiwa vya Pasifiki inayosaini makubaliano ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Pande mbili zinatakiwa kuimarisha kuunganisha mkakati wa maendeleo ndani ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuanzisha mazungumzo ya biashara huria mapema iwezekanavyo, kujitahidi kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika sekta za uwezo wa uzalishaji, biashara, uwekezaji na uvutiaji wa mitaji.

    Bw. Peter O'Neill amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litasaidia kuimarisha mawasiliano na ujenzi wa miundo mbinu kati ya nchi za visiwa vya Pasifiki, Papua New Guinea itashiriki kwenye ujenzi wa pendekezo hilo.

    Rais Xi na waziri mkuu Peter O'Neill wamehudhuria uzinduzi wa Barabara ya uhuru na shule ya Butuka. Rais Xi amesema, barabara ya Uhuru inaunganisha urafiki kati ya watu wa China na Papua New Guinea, pia inabeba matumaini mema ya watu wa China kwa watu wa Papua New Guinea. Anaamini kwamba, barabara hiyo italeta urahisi na ustawi kwa wenyeji.

    "kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya China na nchi zinazoendelea ni chaguo la kimkakati la China kwa muda mrefu, tunapenda kushirikiana na Papua New Guinea kuimarisha hali ya kuaminiana, kupanua maingiliano, kuimarisha ushirikiano, na kupanga na kujenga kwa pamoja njia ya ustawi, njia ya kufungua mlango na njia ya urafiki."

    Shule ya Butuka pia ina jina la shule ya urafiki kati ya China na Papua New Guinea, ni mradi wa kunufaisha raia wa nchi hiyo unaojengwa na China, ambayo itawawezesha wanafunzi zaidi elfu 3 kuingia shuleni.

    Rais Xi amesema China kujenga shule hiyo ni kwa ajili ya kuisaidia Papua New Guinea kuwaandaa watu. Anaamini watu wenye ujuzi watatoa uungaji mkono kwa nchi hiyo kutimiza maendeleo endelevu.

    "msingi muhimu zaidi wa uhusiano kati ya China na Papua New Guinea ni kuenzi urafiki. Natumai vijana wa nchi hizo mbili wataigana, kuzidisha maelewano, na kuwa warithi na watekelezaji wa urafiki kati ya nchi hizo mbili. Naamini vijana wa nchi hizo mbili hakika watajenga mustakabali mzuri zaidi wa China na Papua New Guinea. "

    Bw. Peter O'Neill amesema, mradi wa Shule ya Butuka ni mfano mzuri mwingine wa uhusiano wenye nguvu kati ya Papua New Guinea na China, anaamini ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya nchi hizo mbili utaimarika zaidi, kupanuka zaidi, na kuhimiza zaidi maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako