• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Programu mpya kwa mama mboga yaundwa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-11-16 18:29:38

    Programu ya simu ya mkononi ambayo inawaunganisha mama mboga na wanunuzi imeundwa nchini Uganda.

    Programu hiyo ambayo pia inapatikana katika mtandao wa intaneti iliyopewa jina la @Mboga safi mlangoni kwako@ inawalenga watu binafsi,hoteli na taasisi ,na inaongeza mauzo ya mama mboga katika masoko ya jijini Kampala.

    Huduma hizo baadae zitasambazwa katika maeneo mengine nchini Uganda.

    Programu hiyo iliundwa na Taasisi ya Mabadiliko ya Kijamii (ITS) kwa ushirikiano na ubalozi wa Uswidi na Umoja wa Mataifa ili kuwawezesha wanawake kukumbatia biashara za kielektroniki.

    Uvumbuzi huo unamuwezesha mnunuzi kulipa pesa taslimu au kwa njia ya simu.Baada ya kuagiza bidhaa na kueleza sehemu ya bidhaa kupelekwa,mfumo wa uchukuzi wa Uber,Taxify au Bodaboda unapeleka bidhaa hizo hadi sehemu husika.

    Programu hiyo itazinduliwa tarehe 15 Desemba,2018 baada ya wanawake kupewa mafunzo kuhusu jinsi inavyofanya kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako