• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki ya KCB yasifia usimamizi bora kwa mafanikio yake. (Kwa hisani ya Taifa Leo)

    (GMT+08:00) 2018-11-16 20:12:20

    Benki ya Kenya Commercial imetangaza ongezeko la faida la asilimia 20 katika muda wa miezi tisa kufikia Septemba 30, 2018 ikilinganishwa na wakati huo mwaka wa 2017. Katika taarifa, KCB ilisema ongezeko la faida hiyo ni kutokana na usimamizi mzuri wa gharama na kuimarika kwa mapato yanayotokana na riba. Kulingana na taarifa hiyo mapato nje ya matawi yaliendelea kuongezeka na kwa sasa ni asilimia 87 ya mapato yake ikilinganishwa na asilimia 13 yaliyopatikana katika matawi yake.

    Matumizi ya huduma zake kupitia kwa mawakala yaliongezeka kwa asilimia 74 ilhali idadi ya wananchi waliopata huduma za benki kwa njia ya simu iliongezeka kwa asilimia 34, matumizi ya ATM na maeneo ya kutoa yaliongezeka kwa asilimia 36 na 16 kwa mfuatano huo. Gharama ya operesheni ilipungua kwa Sh2.1 bilioni kutokana na kupungua kwa gharama ya wahudumu wake na mikopo mibaya. Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano ilionyesha kuwa kiwango cha kuhifadhi pesa humo kimeongezeka kwa asilimia 6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako