• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yaipongeza China kwa kupiga marufuku uuzaji wa pembe za ndovu.

    (GMT+08:00) 2018-11-16 20:12:48

    Serikali ya Kenya imepongeza serikali ya Uchina kwa kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kuondoa marufuku ya biashara ya pembe za kifaru na ngozi ya chui. Serikali ya China ilibatilisha uamuzi huo Jumatatu Novemba 12 kupitia kwa Baraza la Serikali. China ilikuwa imeondoa marufuku hayo ya miaka 25 kwa kusema sehemu hizo ni muhimu katika utengenezaji wa dawa. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Utalii Bw Mulei Muia, marufuku hayo ni hatua nzuri kwa sababu ni muhimu kwa uhifadhi wa wanyama walio katika hatari. Katika muda wa miaka 25 ambapo marufuku hayo yamekuwa, idadi ya aina ya wanyama hao imeongezeka.Kulingana na wizara hiyo, serikali imejitolea kufanya kazi na serikali ya China kuhifadhi na kulinda wanyama na rasilimali ya porini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako