• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na viongozi wa nchi za visiwa vya Pasifiki

    (GMT+08:00) 2018-11-16 21:17:42

    Rais Xi Jinping wa China huko Port Moresby amekutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa nchi za visiwa vya Pasifiki.

    Rais Xi amekutana na mwenzake wa Micronesia Bw. Peter Christian na kutumai pande mbili kutekeleza makubaliano ya ushirikiano ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuhimiza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo na uvuvi, ujenzi wa miundombinu na kufanya maandalizi mazuri ya shughuli za mwaka ya utalii ya China na nchi za visiwa vya Pasifiki ya mwaka 2019.

    Alipokutana na waziri mkuu wa Samoa Bw. Tuilaepa Sailele Malielegaoi, Rais Xi amesema, pande mbili zinatakiwa kudumisha hali ya kuamiana ya kisiasa huku zikiendelea kuungana mikono katika masuala muhimu yanayofuatiliwa na nchi hizo mbili na kufanya ushirikiano katika sekta mbalimbali chini ya utaratibu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako