• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa makala kwenye vyombo vya habari vya Brunei

    (GMT+08:00) 2018-11-17 18:27:32

    Kabla ya kufanya ziara nchini Brunei, rais Xi Jinping wa China ametoa makala kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo, ambayo ina kichwa kisemacho "Kushirikiana Kufungua Sura Mpya ya Uhusiano wa China na Brunei".

    Rais Xi amesema, tangu China na Brunei zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1991, na kuanzisha uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati miaka mitano iliyopita, hali ya kuaminiana kati ya pande hizo mbili imeongezeka, ushirikiano umetekelezwa kwa hatua madhubuti, na pande mbili zimeungana mkono katika mambo ya kimataifa na ya kikanda. Pendekezo la kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limeungwa mkono na Brunei, pande mbili zimesaini nyaraka za makubualiano, kuhimiza pendekezo hilo kuuganishwa na mpango wa mwaka 2035 wa Brunei, na kutia nguvu mpya kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili.

    Rais Xi pia amesema, pande mbili zinapaswa kuinua hali ya kuaminiana ya kisiasa, kuzidisha ushirikiano, kuongeza maingiliano kati ya watu na watu, na kuimarisha uratibu katika mambo ya kimataifa na ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako