• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaidia nchi za visiwa vya Pasifiki kuingia kwenye jukwaa la siasa la kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-11-17 18:29:17

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Papua New Guinea jana alikutana na viongozi wa nchi za visiwa vya Pasifiki ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China, na kubadilishana nao maoni kuhusu uhusiano kati ya China na nchi hizo, pamoja na kutoa mapendekezo manne ya "kuzidisha hali ya kuaminiana, kustawi kwa pamoja, kuongeza urafiki na kusaidiana kulinda haki na usawa", na kuanzisha zama mpya ya uhusiano kati ya China na nchi hizo.

    Nchi za visiwa vya Pasifiki zimepata uhuru kutoka utawala wa kikoloni muda si mrefu uliopita, uchumi wao uko katika kipindi cha mwanzo cha kuendeleza viwanda. Zinapata msaada wa kiuchumi kutoka kwenye nchi zilizozitawala, huku zikidhibitiwa kisiasa.

    China inashikilia kanuni ya kuheshimu watu wa nchi za visiwa vya pasifiki kuchagua wenyewe njia ya kujiendeleza, kutoa msaada usio na sharti lolote la kisiasa kadiri iwezavyo, na kuweka umuhimu kwenye maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi hizo.

    Nchi za magharibi pia zinaigiza China kuongeza uwekezaji na msaada katika kanda ya Pasifiki ya Kusini, na kujaribu kupunguza ushawishi wa China katika sehemu hiyo.

    China haijali msaada wa nchi za magharibi, kama msaada huo utatolewa, hakika utahimiza maendeleo ya sehemu hiyo. Lakini wanasiasa wa nchi za magharibi hawakutarajia kuwa, mbunge wa Papua New Guinea angesema ni uungaji mkono na uhusiano kati yake na China, ndio umesaidia Papua New Guinea kuingia kwenye jukwaa la siasa la kimataifa.

    Ikilinganishwa na nchi za magharibi, msaada wa China kwa nchi za visiwa vya Pasifiki umehusiana katika pande mbalimbali. Rais Xi Jinping wa China ameahidi kuwa, China itafungua soko lake kwa nchi hizo, kupanua uwekezaji na kuzidi kununua bidhaa za nchi hizo. Rais Xi amesema China inaunga mkono nchi za visiwa vya Pasifiki kutoa sauti yao, kuunga mkono nchi hizo kusukuma mbele pendekezo la "Pasifiki ya Buluu", kuimarisha mawasiliano na uratibu na nchi hizo katika mambo ya kimataifa, kusaidiana na kushirikiana kwa kulinda haki na usawa wa kimataifa.

    Viongozi wa nchi za visiwa vya Pasifiki pia wameeleza imani yao kwamba, China ni mwenzi muhimu wa nchi hizo katika kutimiza mustakabali wa kujiendeleza, kuongeza manufaa kwa wananchi wao na kukabiliana na changamoto za dunia, na kusema wanapenda kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Uhusiano kati ya China na nchi za visiwa vya Pasifiki umeingia kwenye kipindi kipya cha ushirikiano wa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako