• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utatuzi wa China waonyesha mwelekeo wa maendeleo ya Asia na Pasifiki

    (GMT+08:00) 2018-11-17 20:11:47

    "Tuko kwenye meli moja", rais Xi Jinping wa China leo ametumia maneno hayo alipoanza hotuba yake kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa APEC. Kwenye hotuba yake, rais Xi ametetea kushikilia kufungua mlango, kujiendeleza, ushirikiano shirikishi, uvumbuzi na kanuni, kutoa "utatuzi wa China" juu ya namna inavyoshika mwelekeo sahihi wa maendeleo ya uchumi wa dunia, na kupata wazo la usimamizi wenye ufanisi kwa makundi ya uchumi ya Asia na Pasifiki.

    Kwenye ramani ya uchumi wa dunia, Asia na Pasifiki ni sehemu hai ya ongezeko na uwezo wa maendeleo. Kwa sasa, GDP ya makundi 21 ya uchumi wa APEC imechukua asilimia 60 ya dunia, thamani ya biashara imechukua asilimia 47 ya dunia nzima. Mafanikio hayo yanatokana na Lengo la mwaka 2020 lililothibitishwa kwenye mkutano wa APEC uliofanyika mjini Bogor mwaka 1994 na kushikilia biashara huria na kurahisisha uwekezaji.

    Hivi sasa, ushirikiano kati ya makundi ya uchumi ya APEC umefika njia panda, unapata fursa ya mageuzi ya teknolojia mpya na mageuzi ya viwanda, pia unakabiliwa na changamoto za kuongezeka kwa biashara huria, kurudi nyuma utandawazi wa dunia na usimamizi mbaya wa uchumi. Hivyo rais Xi kwenye hotuba yake ameeleza kuwa, masuala ya kushirikiana au kupambana, kufungua mlango au kufungwa, kunufaishana au kutonufaishana, yanahusiana na maslahi ya nchi mbalimbali na mustakabali wa binadamu.

    Miaka 40 tangu China ilipoanza kufanya mageuzi na kufungua mlango, China siyo tu imetoa wazo, bali pia ina hatua halisi katika kuhimiza maendeleo ya Asia na Pasifiki. Mwaka 2016, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi wanachama wa APEC imechukua asilimia 62 ya biashara yote ya China, uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwa nchi wanachama wa APEC umechukua asilimia 72 ya uwekezaji wote wa China katika nchi za nje. China imekuwa nguvu muhimu ya kuhimiza ushirikiano wa maendeleo ya Asia na Pasifiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako