Ayatollah amesema Iraq rafiki, yenye nguvu, huru na yenye maendeleo itakuwa na manufaa zaidi kwa Iran, na watu wa Iran watasimama pamoja na wairaq.
Rais Salih amesema ni fahari kwake kukutana na Ayatollah Khamenei, na kukumbusha kuwa amefanya ziara nchini Iraq kuthibitisha kuwa uhusiano kati ya Iraq na Iran unatokana na historia, na hautabadilika. Amesema Iraq inatarajia kuiga uzoefu wa Iran kwenye ujenzi mpya wa Iraq.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |