• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahutubia mkutano wa 26 usio rasmi wa viongozi wa APEC

    (GMT+08:00) 2018-11-18 17:00:07
    Mkutano wa 26 usio rasmi wa viongozi wa APEC umefanyika leo huko Port Moresby, Papua New Guinea. Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba yenye kichwa cha "kutumia fursa ya zama, na kutafuta kwa pamoja ustawi wa Asia na Pasifiki", akisisitiza kuwa pande mbalimbali zinapaswa kufuata mwenendo wa maendeleo ya utandawazi wa uchumi, kushikilia lengo la kuhimiza mafungamano ya kikanda, kufuata mwelekeo wa kujenga uchumi ulio wazi wa duniani, kujitahidi kudumisha ushirikiano wa Asia na Pasifiki, na kuingia kwenye kiwango cha juu zaidi kwa madhubuti.

    Rais Xi Jinping ametoa mwito wa kuendelea na mafungamano ya kikanda, kujenga uchumi ulio wazi wa Asia na Pasifiki, kuendelea kuhimiza uchumi kwa uvumbuzi na kuandaa nguvu mpya za ongezeko la uchumi, kushikilia kukamilisha mtandao wa mawasiliano na kuhimiza maendeleo shirikishi, na kushikilia kuzidisha uhusiano wa kiwenzi na kushirikiana kukabiliana na mchakato za pamoja.

    Pia amesema, viongozi wa sehemu ya Asia na Pasifiki wana jukumu la kupanga mustakabali wa ushirikiano baada ya mwaka 2020 wa APEC. China itashiriki kwa kina kwenye mchakato wa ushirikiano wa APEC, kutoa mchango mpya kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya sehemu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako