• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha kauli ya makamu wa rais wa Marekani kuhusu China kuongeza mzigo wa madeni kwa nchi za visiwa vya Pasifiki

    (GMT+08:00) 2018-11-18 17:00:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema maoni ya rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa viongozi wa APEC yanaendana na mwelekeo wa maendeleo ya usimamizi wa uchumi wa dunia, kuendana na matumaini ya jumuiya ya kimataifa, na yamekubaliwa na pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo.

    Bibi Hua Chunying amesema APEC iko katika kipindi muhimu cha maendeleo, huku pande mbalimbali zinapaswa kuonyesha msimamo wa kubeba majukumu, kukumbuka lengo la kuanzisha jumuiya hiyo, kufuata mwelekeo wa maendeleo ya Asia na Pasifiki.

    Pia amesema, China inapendekeza nchi husika zisiingilie mambo ya nchi nyingine, kuzitendea kwa usawa nchi kubwa na ndogo, kuheshimu haki za nchi nyingine kuchagua njia ya kujiendeleza, na kutekeleza kihalisi kwa mujibu wa maendeleo ya nchi zinazoendelea.

    Makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence amehutubia mkutano wa viongozi wa viwanda na biashara wa APEC, akisema msaada wa China kwa nchi za visiwa vya Pasifiki umeongeza mzigo wa madeni kwa nchi hizo, kauli hiyo imekanushwa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako