• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meli ya ushirikiano wa Asia na Pasifiki yang'oa nanga tena

    (GMT+08:00) 2018-11-18 21:20:57

    Mkutano wa 26 usio rasmi wa viongozi wa APEC umefungwa leo huko Port Moresby, Papua New Guinea. Makundi ya uchumi ya jumuiya hiyo yamefikia makubaliano katika kuhimiza mawasiliano, ujenzi wa biashara huria ya Asia na Pasifiki, uchumi wa kidigitali na mpango baada ya kutimizwa kwa "Lengo la Bogor".

    Rais Xi Jinping wa China ametetea kushikilia kufungua mlango, kujiendeleza, ushirikiano shirikishi, uvumbuzi na kanuni, na kukubaliwa na pande mbalimbali. Amesema China inaamini kuwa, "utatuzi wa China" utachochea ushirikiano wa Asia na Pasifiki katika siku za usoni.

    Kwa sasa meli ya maendeleo ya Asia na Pasifiki imeng'oa nanga tena, na kutunga mpango baada ya kutimizwa kwa "Lengo la Bogor" ni sehemu nyingine ya meli hiyo inayokwenda. Hivyo, China imependekeza kujenga eneo la biashara huria lenye kiwango cha juu, mawasiliano ya pande zote na uchumi wa kidigitali, ili kuhakikisha mustakabali wa Asia na Pasifiki. Mchakato wa ushirikiano wa Asia na Pasifiki unakabiliana na changamoto, wakati utaratibu wa uchumi duniani unabadilika. Makundi hayo yanapaswa kuendelea kufungua mlango, kufanya uvumbuzi na ushirikiano shirikishi, ndipo yanaweza kuendesha kwa pamoja meli hiyo kuelekea mustakabali mzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako