• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA WANAWAKE: AWCON 2018: Starlets wafungashiwa virago

    (GMT+08:00) 2018-11-19 08:32:59
    Timu ya soka ya taifa ya soka ya wanawake nchini Kenya (Harambee Starlets) imefungashiwa virago katika michuano ya kombe la Afrika la wanawake (AWCON) mwaka huu baada ya rufaa yake kutupiliwa mbali na mahakama ya kusikiliza michezo (CAS).

    Shirikisho la soka la Kenya (FKF) limesema halitochoka kutafuta haki, na kuwa rufaa yao bado iko wazi na kuwataka Wakenya kuwa watulivu kipindi hiki.

    Mashindano ya AWCON yatatumika kuchagua wawakilishi watatu wa Bara Afrika katika Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Ufaransa mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako