• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: RT yamtambulisha mkufunzi mpya

    (GMT+08:00) 2018-11-19 08:33:19
    Shirikisho la riadha Tanzania (RT) limemtambulisha mkufunzi mpya Ayane Sato kutoka nchini Japan. Mkufunzi huyo amewasili nchini humo kupitia ushirikiano uliopo kati ya serikali ya Tanzania na Japan.

    Akizungumza na waandishi wa habari, katibu msaidizi wa RT Ombeni Zavala amesema kocha huyo atajikita kutoa mfunzo ya mbio fupi, za kati, miruko na mitupo.

    Kocha huyo ataanza kutoa mafunzo Novemba 27 kwa walimu wa riadha kabla ya kuwafikia wanariadha ili kuhakikisha nchi hiyo itashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Olimpiki ya Tokyo 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako