• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kimetto na Chepchirchir kupigania ubingwa wa Shanghai Marathon

    (GMT+08:00) 2018-11-19 08:33:38
    Mabingwa wa zamani wa Tokyo Marathon, Dennis Kimetto (mwaka 2013) na Sarah Chepchirchir (2017) wametoa ithibati ya kupigania ubingwa wa mbio za Shanghai Marathon yaliyoanza jana hapa China katiika jiji la Shanghai.

    Macho yatakuwa kwa Kimetto ambaye hajamaliza mbio za kilomita 42 tangu akamilishe London Marathon nchini Uingereza katika nafasi ya tisa mwezi Aprili mwaka 2016.

    Wapinzani wake wakuu ni Mkenya Asbel Kipsang' na Waethiopia Yitayal Atnafu, Seyefu Tura na Tsegaye Mekonnen.

    Chepchirchir anatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Mkenya Flomena Cheyech na Waethiopia Yebrgual Melese na Helen Tola Bekele. Rekodi ya Shanghai Marathon ya wanawake inashikiliwa na Muethiopia Tigist Tufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako