• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la Gallabant Mashariki mwa Sudan latajwa kutokomeza Usubi

    (GMT+08:00) 2018-11-19 08:58:30

    Wizara ya afya ya Sudan imetangaza kuwa eneo la Gallabant lililopo kwenye jimbo la Qadarif mashariki mwa nchi hiyo, kwenye mpaka na Ethiopia limeondokana na hatari ya ugonjwa wa usubi. Waziri wa afya wa Sudan Bw. Mohamed Abu Zaid, amesema Sudan imefanikiwa kuzuia kuendelea kwa ugonjwa huo, baada ya kutokomeza katika eneo la Abu Hamad kaskazini mwa nchi hiyo.

    Amefafanua kuwa ushirikiano kati ya Sudan na Ethiopia, umechangia kuwa na matokeo mazuri, na watu laki 1.5 wa eneo hilo sasa hawahitaji tena matibabu.

    Ofisa Mkuu mtendaji wa Kituo cha Carter chenye makao yake mjini Atlanta, Bibi Mary Ann, amesema kituo chake kitaendelea kupambana na ugonjwa huo nchini Sudan. Amewataka wadau wa afya kuendelea na juhudi za kupambana na ugonjwa huo katika nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako