• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika walenga kuhimiza amani na usalama kwa juhudi mpya

    (GMT+08:00) 2018-11-19 08:58:51

    Kuzinduliwa kwa mfuko wa amani wa Umoja wa Afrika, kumetajwa kuwa ni sehemu ya juhudi za umoja huo kuhimiza amani barani Afrika. Mfuko huo ambao umezinduliwa kwenye mkutano wa 11 wa Umoja wa Afrika uliofanyika huko Addis Ababa, utajikita kwenye maeneo matatu, ambayo ni upatanishi na demokrasia ya kuzuia migogoro, uwezo wa kitaasisi na kuunga mkono operesheni za usalama.

    Tayari mfuko huo umechagua wajumbe watano wa bodi na meneja wake, na unatarajiwa kuanza kwa bajeti ya dola milioni 100 za kimarekani. Kwenye uzinduzi wa mfuko huo, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema tayari nchi wanachama zimechangia dola milioni 60 kwenye mfuko huo.

    Mwenyekiti wa kamati ya umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat, amesema, wadau wengine wawili wa umoja huo yaani Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya, watashiriki kwenye usimamizi wake, na wajumbe wa bodi waliochaguliwa watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano, kusimamia matumizi ya fedha za mfuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako