• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika kusini kuteua mwendesha mashtaka mkuu ndani ya muda uliowekwa na mahakama ya katiba

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:00:56

    Ikulu ya Afrika Kusini imesema rais Cyril Ramaphosa wa nchi hiyo atateua mkuu wa Mamlaka ya mashtaka ya taifa NPA ndani ya muda uliowekwa na mahakama ya katiba.

    Msemaji wa rais Bw. Khusela Diko amesema jopo la washauri wanaotakiwa kupendekeza majina ya watu wanaofaa wadhifa huo, wamewasilisha majina matano, na rais Ramaphosa ambaye yuko nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika, atapitia majina hayo na kufanya uteuzi ndani ya muda ulioagizwa na mahakama ya katiba.

    Imefahamika kuwa NPA ikiwa ni taasisi muhimu ya kisheria nchini Afrika kusini, imekuwa haina uongozi wenye ufanisi tangu mwezi Agosti, baada ya mahakama ya katiba kutangaza uteuzi uliotolewa na rais wa zamani Jacob Zuma wa Bw. Shaun Abrahams kuwa mkuu wa NPA, kuwa ni "batili na kinyume na katiba".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako