• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia inafanya juhudi kuitaka Tanzania kuwaachia raia wake 224 wanaoshikiliwa

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:01:36

    Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema Ethiopia inafanya juhudi kuitaka Tanzania iwaachie huru raia wake 224 wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuingia nchini humo kiharamu.

    Wizara hiyo imesema kupitia taarifa kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu na mwenzeke wa Tanzania Bw. Augustine Philip Mahiga walikutana kujadili suala hilo kando ya mkutano wa kilele wa 11 wa Umoja wa Afrika uliofanyika wikiendi iliyopita mjini Addis Ababa.

    Raia 224 wa Ethiopia wanashikiliwa nchini Tanzania wakiwa njiani kuelekea Afrika Kusini. Wafanya magendo ya binadamu wameripotiwa kutumia nchi kadhaa kama vituo vya kuwasafirisha waethiopia kwenda Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako