• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awasili Bandar Seri Begawan kwa ziara nchini Brunei

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:12:03

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Bandar Seri Begawan, na kuanza ziara yake nchini Brunei. Rais Xi amekaribishwa kwa ukarimu kwenye uwanja wa ndege wa Bandar Seri Begawan. Rais Xi amesisitiza kuwa, China na Brunei ni majirani wema, marafiki na wenzi wa kuaminiana, na mawasiliano ya kirafiki kati yao yana historia ndefu.

    Amesema tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 27 iliyopita, zimetendeana kwa usawa, kiwango cha kuaminiana kisiasa kati yao kimeinuka, ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili na kutoa mchango mkubwa kwa amani na ustawi wa kanda hiyo.

    Rais Xi amesema anatumai kuwa ziara yake itaenzi na kuhimiza urafiki wa jadi kati ya China na Brunei, kupanga kwa pamoja mustakbali wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika zama mpya, na kuufanya uhusiano wa kirafiki na ujirani mwema kati ya nchi hizo mbili uinuke kwenye ngazi mpya, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako