• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Houthi la Yemen watangaza kusimamisha mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia na UAE

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:12:27

    Waasi wa Houthi wa Yemen wametangaza kusimamisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Saudi Arabia na UAE. Mkuu wa kamati kuu ya mageuzi ya kundi hilo Bw. Mohammed Ali al-Houthi ametoa taarifa akisema hatua hiyo inatekelezwa kwa kutikia wito wa mjumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Yemen Bw. Martin Griffiths, ambaye amelitaka kundi hilo kusimamisha mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya nchi hizo mbili, ili kuonyesha nia njema kabla ya mazungumzo ya amani.

    Habari kutoka shirika la habari la SABA zinasema, kundi la Houthi limesema mtoto mmoja ameuawa kwenye shambulizi la kikosi cha muungano kinachoongozwa na Saudi Arabia katika mkoa wa Saada, kwenye mpaka wa kaskazini, na mtoto mwingine amejeruhiwa kwenye shambulizi dhidi ya kijiji cha Ghafirah, katika eneo la Dhahir.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako