• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi wa misaada nchini Sudan Kusini watarajia amani itarahisisha kazi zao

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:52:44

    Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini waliokumbwa na migogoro ya miaka mitano, wanatarajia hali ya usalama itaendelea kuboreka ili waweze kufikisha misaada kwa maelfu ya watu wenye mahitaji ya dharura.

    Msemaji wa Shirika la misaada ya kibinadamu la Afrika SAADO Bw. Junior Ali amesema, ingawa hana hakika kuwa hali ya amani ya sasa itaendelea kwa muda gani, lakini anatarajia mambo mazuri yatakuja. Anaona, hivi sasa, kazi zao zimebadilika kutoka kushugulikia hali ya dharura, na kuwa kujenga makazi, barabara na shule nzuri kwa ajili ya jamii.

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake Bw. Riek Machar walisaini makubaliano ya amani kuanzia tarehe 12, mwezi wa Septemba nchini Ethiopia, ambayo waangalizi wanaamini yataheshimiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako