• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Lendu la DRC lawauwa wavuvi wawili wa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-11-19 09:54:26

    Wavuvi wasiopungua wawili wa Uganda wameuawa, mmoja kujeruhiwa na wengine sita hawajulikani walipo baada ya kundi la wapiganaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufanya mashambulizi katika ziwa Albert la mpakani kati ya Uganda na DRC.

    Kamanda wa polisi wa jimbo la Albertine Bw. Deo Obura, amesema kundi hilo la Lendu la DRC limedai wavuvi hao waliingia kwenye eneo linalodhibitiwa nao na kufanya uvuvi haramu.

    Siku tano zilizopita, kundi hilo pia liliwaua wavuvi watano wa Uganda na kuikatakata miili yao na kuitupa katika ziwa hilo.

    Habari zinasema kundi hilo linalinda eneo la maji yake dhidi ya wavuvi haramu kutoka Uganda.

    Uganda na Congo zimewahi kukubaliana kufanya operesheni za pamoja kuzuia mapambano ya kugombea eneo na uvuvi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako