• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarusha satilaiti mbili mpya za mfumo wa Beidou

    (GMT+08:00) 2018-11-19 10:52:08

    China imerusha satilaiti mbili mpya za Mfumo wa Satilaiti za Kuongoza Mawasiliano wa Beidou kwenye anga ya juu kwa kutumia roketi aina ya Long March-3B kutoka kwenye Kituo cha Kurushia Satilaiti cha Xichang mkoani Sichuan saa 8: 07 leo alfajiri kwa saa za Beijing. Satilaiti hizo ziliingia kwenye njia zilizopangwa za kuizunguka dunia baada ya kusafiri kwa masaa matatu, na zitaungana na satilaiti nyingine 17 za Mfumo wa Beidou Namba 3 kwenye anga ya juu, utakaotoa huduma za kuongoza mawasiliano kwa nchi na sehemu zilizojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kabla ya mwisho wa mwaka huu. Satelaiti hizo mbili pia ni ya 42 na ya 43 ya mfumo wa satelaiti za Beidou zilizorushwa kwenye anga ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako