• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa makala kwenye magazeti ya Ufilipino

    (GMT+08:00) 2018-11-19 12:49:06

     

    Rais Xi Jinping wa China ametoa makala yenye kichwa cha "Kujenga mustakabali mpya wa uhusiano kati ya China na Ufilipino" kwenye magezeti ya Ufilipino kabla ya kuanza ziara yake nchini humo.

     

    Rais Xi amesema, katika ziara hiyo anatarajia kubadilishana maoni na rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino kuhusu jinsi ya kuinua ushirikiano wa pande zote kati ya nchi zao katika mazingira mapya, na kupanga mipango na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo kwenye kiwango cha juu zaidi. Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuimarisha uaminifu wa kisiasa, kufanya ushirikiano kwa vitendo, kudumisha mawasiliano kati ya wananchi na kuhimiza maendeleo ya ushirikiano katika kanda ya Asia Mashariki.

     

    Rais Xi ameongeza kuwa, China ni nchi inayowajibika, na inashikilia ushirikiano wa kutafuta mafanikio kwa pande zote, kupanua ufunguaji mlango, na kuchangia fursa na nguvu za soko lake na nchi nyingine.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako