• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na sultani wa Brunei

    (GMT+08:00) 2018-11-19 18:34:28

    Rais Xi Jinping wa China huko Bandar Seri Begawan, mji mkuu wa Brunei amekutana na sultani Haji Hassanal Bolkiah wa nchi hiyo. Viongozi hao wamepongeza mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbi, huku wakiamua kujenga uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya nchi na kuwa wenzi wenye maelewano ya kisiasa, ushirikiano wa kiuchumi wa kunufaishana, mawasiliano ya utamaduni wa kibinadamu, uhusiano wa kusaidiana.

    Sultani Hassanal amemkaribisha rais Xi kwa ziara yake ya kwanza nchini Brunei huku akisema, ziara hiyo itazidisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande mbili katika sekta mbalimbali.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China inaichukulia Brunei kama mwenzi muhimu wa ushirikiano wa kujenga njia ya Hariri Baharini ya karne 21, huku ikipenda kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" la China na mkakati wa maendeleo wa "Malengo ya 2035" wa Brunei ili kuendeleza viruzi ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

    Baada ya mkutano huo, viongozi hao wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirkiano wa pande mbili ukiwemo ujenzi wa pamoja wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako