• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema makubaliano ni kanuni ya msingi ya nchi wanachama kushiriki kwenye ushirikiano wa APEC

    (GMT+08:00) 2018-11-19 18:55:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mazungumzo na makubaliano ni kanuni ya msingi ya nchi wanachama kushiriki kwenye Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC, ambayo pia ni sharti la msingi la maendeleo ya shirika hilo.

    Amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano na pande mbalimbali ili kusukuma mbele ushirikiano wa APEC na kushiriki kwenye mjadala wa masuala husika.

    Kauli hiyo inatokana na mkutano usio rasmi wa 26 wa viongozi wa shirika la APEC kushindwa kutoa azimio la viongozi kabla ya kufungwa.

    Bw. Geng amesema, pande mbalimbali zinatakiwa kuheshimiana na kuvumiliana, na kuhimiza ushirikiano wenye ufanisi chini ya msingi wa mazungumzo na makubaliano, ili kuhimiza ustawi wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako