• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: AWCON WANAWAKE: Zambia yaiangusha Equitorial Guinea

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:40:34
    Timu za taifa za mchezo wa soka wa wanawake za Zambia, Afrika Kusini, Ghana na Camroon zimeanza vyema kwenye michuano ya 11 kuwania taji la bara la Afrika upande wa wanawake (AWCON)

    Fainali hizo zilianza mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Ghana, Zambia imepata ushindi mnono wa magoli 5-0 na kuwashangaza Equatorial Guinea ambao walielemewa vibaya.

    Matokeo mengine ya kundi B, mabingwa watetezi Nigeria wamelazwa na Afrika Kusini kwa bao 1-0, huku wenyeji Ghana wakiibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Algeria, na Cameroon wakiwashinda Mali mabao 2-1.

    Washindi watatu wa kwanza wataliwakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia mwakani jijini Paris Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako