• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mwanasoka bora wa BBC: Salah, Mane, Koulibaly, Benatia na Partey kutunishiana misuli

  (GMT+08:00) 2018-11-20 08:41:39

  Orodha ya wanasoka watakaowania tuzo ya mwanasoka bora wa BBC barani Afrika mwaka wa 2018 imetangazwa. Wawaniaji watakuwa Medhi Benatia (Morocco), Kalidou Koulibaly (Senegal), Sadio Mane (Senegal), Thomas Partey (Ghana) na Mohamed Salah (Misri).

  Shughuli za kupigia kura waliotajwa kupitia mitandao ya kijamii ilianza Jumamosi Novemba 17 na itafungwa rasmi Jumapili Disemba 2 kabla ya mshindi kutangazwa rasmi Ijumaa, Disemba 14.

  Mshambulizi wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah ndiye alishinda tuzo hiyo mwaka wa 2017, mwaka uliomshuhudia akihama Roma ya Italia hadi ligi ya EPL na baadaye akaliongoza taifa lake kushiriki fainali ya kwanza la Kombe la Dunia tangu mwaka wa 1990.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako