• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan asema ataendelea kuunga mkono juhudi za amani barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:52:09

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema nchi yake itaendelea kufanya juhudi kuleta amani na utulivu barani Afrika. Akiongea na Rais Obiang Nguema wa Jamhuri ya Ikweta, anayefanya ziara ya siku mbili nchini Sudan, Rais al-Bashir amesema kwa miaka yote Sudan imekuwa makini kuhimiza usalama na utulivu barani Afrika, na hasa kwenye nchi jirani.

    Rais Nguema amesema nchi yake inapenda kuimarisha uhusiano kati yake na Sudan kwenye maeneo yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako