• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaimairisha usalama kwenye mpaka kati yake na Somalia baada ya kuvunja jaribio la shambulizi

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:52:29

    Inspekta Jenerali wa polisi wa Kenya kamanda Joseph Boinnet, amesema Kenya imeimarisha usalama kwenye mpaka wake na Somalia na kuongeza idadi ya polisi, baada ya polisi kuvunja jaribio la shambulizi la wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.

    Polisi wamechukua hatua hiyo baada ya wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab kujaribu kushambulia kambi ya polisi kwenye eneo la Ijara, Boni. Wapiganaji wanne wameuawa kwenye shambulizi hilo lililotokea alfajiri ya jana.

    Kamanda Boinnet amesema wapiganaji hao walikuwa wakilenga miundombinu ya mawasiliano, wakati walipojaribu kushambulia kambi ya polisi wa kufanya doria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako