• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafanya majadiliano kuhusu makubaliano 35 ya huduma za ndege ili kuimarisha sekta ya usafiri wa ndege

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:52:52

    Kenya inapanga kufanya majadiliano kuhusu makubaliano 35 na nchi mbalimbali, ili kuimarisha sekta yake ya usafiri wa ndege. Akiongea mjini Nairobi, Mkurugenzi wa mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya Bw. Gilbert Kibe, amesema kwenye mkutano wa 11 wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO) wa majadiliano kuhusu huduma za ndege (ICAN2018) unaofanyika kwa mara ya kwanza katika eneo la Afrika mashariki na kati, Kenya imeomba kufanya majadiliano na nchi 35 wadau, kuangalia upya au kufanyia marekebisho makubaliano yaliyopo.

    Mkutano huo utafanyika mjini Nairobi katikati ya mwezi ujao, na watu 800 wanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo.

    Habari pia zinasema Kenya inapanga kupunguza uchafuzi kwenye sekta ya usafiri wa ndege, ili kuhimiza hali ya kuwa na mazingira endelevu. Bw. Kibe amesema wanayahimiza mashirika ya ndege kutumia mafuta kwa njia zenye ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako