• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda imeimarisha usalama kwenye mpaka wake wa ziwa na DRC

    (GMT+08:00) 2018-11-20 08:53:10

    Uganda imeimarisha usalama kwenye mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ili kuepusha mapambano ya kulipiza kisasi baada ya mauaji na matukio ya utekaji nyara yaliyotokea wikiendi kwenye mpaka huo.

    Msemaji wa polisi wa eneo la Albertine Bw. Julius Hakiza, amesema polisi na wanajeshi wamewekwa kwenye eneo hilo, na doria zimeongezeka kwenye eneo la maji ya ziwa linalogombewa.

    Hatua za usalama zimeimarishwa baada ya wavuvi wa Uganda kupanga kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi, baada ya wanamgambo wa kabila la Lendu kufanya shambulizi lililosababisha vifo vya waganda wawili, kumjeruhi mmoja na wengine sita hawajulikani walipo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako