• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa mwito wa juhudi za kimataifa kurejesha mazungumzo kati ya Palestina na Israel

    (GMT+08:00) 2018-11-20 09:15:17

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu jana ametoa mwito wa juhudi za kimataifa ili kurejesha mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

    Amesema jumuiya ya kimataifa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ni lazima wawe na wajibu na uharaka wa kufanya duru mpya ya juhudi za kuhimiza amani.

    Bw. Ma Zhaoxu pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa mapambano kati ya Palestina na Israel katika ukanda wa Gaza.

    Habari zinasema, wapalestina wasiopungua 25 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya waandamanaji wa Palestina na askari wa Israel kaskazini mwa Gaza, karibu na mpaka na Israel.

    Msemaji wa wizara ya afya ukanda wa Gaza Bw. Ashraf al-Qedra amesema kuwa, majeruhi wamepelekwa hospitali lakini hawakujeruhiwa vibaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako