• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yachukua hatua kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wote kabla mwaka 2030

    (GMT+08:00) 2018-11-20 09:15:45

    Serikali ya Rwanda imechukua hatua ili kutimiza lengo la kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote ifikapo mwaka 2030, kwa kulingana na malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.

    Waziri wa afya wa Rwanda Bw. Jean-Pierre Nyemazi ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa kutafuta fedha kwa ajili ya huduma za afya kwa wote, akisema hatua hizo ni pamoja na kupanua bima ya afya kwa msingi wa jamii "Mutelle de sante", ambao kwa sasa umewamefikia asilimia 90 ya watu.

    Amesema, Rwanda itaendelea kupanua mtandao wa wafanyakazi wa afya katika kila kijiji, na kuwa kiungo muhimu kati ya wananchi na vifaa vya afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako